Siri Zake Zagunduliwa

1
934
image pewa.co.ke

Siri za jamaa mmoja ziliweza kujulikana hivi jana. Jamaa wa umri wa mika wa waki hivi, jirani ya baba fulani anayejulikana kijijini humu hakuwa na la kufikiri mara ya pili kwani alikuwa amesha chunguza kwa undani njama za kijana huyo ambaye ni jirani yake. Alikata kauli kupambana naye vilivyo.

Namo jioni hiyo aliketi hapo kando akingojea jamaa huyo ambaye alikuwa amezoea kupitia kwake na mara tu walipatana ana kwa ana na mwenye boma ambaye ni baba ya binti aliyekuwa akimmezea mate jamaa huyo. Penyenye zinasema kuwa jamaa huyo tangia binti ya mzee huyo kurudi likizoni kutoka shuleni amekuwa akipitia kando ya boma hiyo. Kwani hikuwa mazoeya hapo awali jamaa huyo kupita pita hapo walakini mara tu bintiye aliporudi jamaa huyo aliweza kuwa na mazoea ya kupitia pitia hapo. Ilimwezeza mzee huyo kugunduwa siri yakuwa jama huyu anammezea binti yake mate.

Soma pia: Hivi Ndivyo Kidosho Alivyomuaibisha Padre

Na walipopatana ana kwa ana mazungumzo ikawa hivi

“Ewe kijana siri zako nimezigunduwa tayari. Mbona unapita pita hapa kwangu ukielekea kwenu?”

“Hamna shida kwani mimi sifahamu siri unayoisema, njia hii niligunduwa ni fupi kuelekea nyumbani.” Alimjibu baba Yule.

“Ewe kijana wacha kunikoroga marifa, hivi ndo ushajuwa njia hii ikawa fupi, kwa muda wa hizo siku zote hukuwa unapitia hapa, ila tu aliporejea msichana wangu kwa likizo sasa njia imekuwa fupi?’ Alitaka kujua Mzee yule.

“Zako sema sitambui ila, mimi napitia tu, siri hiyo mimi sifahamu ata” Alijitetea Jamaa yule.

Huku akimuelekezea kidole “Haya basi, sikiza kijana nikueleze, onyo hii nakupa wewe, mimi sitakitena kukuona wapitia hapa. Ushaskia? na kama unalo sikio litumie vema. Siri hiyo yakumtongoza mwanangu ikome mara hii. Wafikiri nimeamkia tu leo hii kugunduwa hivi? Kuchunguza nimechunguza, kwahivyo koma mara hii. Nitakapokupata ukipitia hapa tena utakiona kilichomtoa nyoka pangoni.” Alimuonya vikali.

Mzee huyo alikuwa ameshanongonezewa na watu kuwa kunaye jamaa anaye mazoea ya kupita pitia hapo tangia msichana wake arudi kutoka shuleni kwa likizo ndefu na pia alikuwa akimulizia mulizia msichana huyo kama yupo.

Jamaa aliweza kuenda zake bila kutizama nyuma kwani ata kama alijaribu kujitetea siri zake zilikuwa zimeshagunguliwa.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.