Binti Atoa Masharti Zakuolewa kwake

0
1108
picha twitter

Masharti aliyoyatowa Binti humu mjini Kwale yaliweza kuwacha watu wamedua. Penyenye zetu zimetujulisha kuwa binti aliweza kuletana juu na baba yake alipomueleza kuwa binti yake (majina yamefichwa ) ataolewa lini kwani alishamjuwa kijana aliyekuwa nahusiyano na bintiye. Garika la maneno lilipasuka, mara tu alipomueleza kulingana na desturi za kwao iwapo kijana huyo hajuwi basi binti aweze kumujulisha yakuwa itambidi alete ngombe kumi. Watano wa maziwa na watano wawe fahali.

Bindi huyo akuweza kutulia babaye aweze kumaliza kwa hamaki zake aliweza kupinga baba yake. “Kwani wewe ulipeleka ngombe wangabi kwa kina mama? Hebu masharti hayo yapotee kwani mimi nitaolewa nipendavyo . Hamna ngombe watakaoletwa hivi nakujulisha wazi baba. Tamaduni na mila nakusihi yaweke kando. Imefikia wakati tamaduni hizo na mila za mababu kutupiliwa mabali kwani inawazuiya watu wengi kujenga nyumba zao ….”

penda kusoma pia: Baada Ya Miaka Mitatu Ataka Turudiane

Babaye alimkatiza nakumjulisha kuwa “Masharti hayo ndiyo yanayo kuwa kama msingi wa nyumba. Mibaraka yangu kama mzazi pia wahitaji ili uweze kuwa na familia yenye baraka  kwani wewe huoni jinisi tulivyokusomesha hadi ukafikia kiwango ambayo upo sasa?” Alimshauri Mzazi huyo.

Binti yake alizidi kutia pamba masikioni, hakutaka kusikia maneno ya baba yake, alihisi kuwa masharti yale ni yakupitwa an wakati na baada ya kimya kifupi alizidi kujieleza. “Baba sio eti niwakosea wewe na mama heshima lakini ni mimi nitakaye olewa , na nahisi kanakwamba inanifaa niolewe jinis nipendavyo  masharti hayo kwangu mimi nahisi ni mlima kuu. Nikweli kuwa mibaraka yenu nitahitaji lakini isiwe kizungumkuti kuchangia masharti nipasavyo kuolewa. Niwachieni mimi niolewe kulingana na jinsi mimi ninavyo penda.” Aliomba binti yule.

Wakati mazungumzo haya yalikuwa yanaendelea mama yake alikuwa ameenda Kongowea na Baba yake aliweza kukimya kisha kumkumbusha tena jinsi ilivyo wagarimu fedha nyingi kumpeleka binti yao chuo kiku, na kufuzu kwa Digiri ya hisibati. Na mara tu aliposema masharti yale ya kitamaduni hayapaswi kuvunjwa. Binti alifoka na kuamka huku akienda nje kwa kelele na kulalamika akikashifu Masharti hayo ya kitamaduni. Majirani walibakia wakitizama jinsi binti alivyoenda. Inasemaekana tangia sasa binti huyo ajarejea nyumbani na wazazi wanamuomba arejee nyumbani warekebishe maneno. Msaidizi wa kazi za nyumba alitokea jikoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.